Storm FM

Wasabato wafanya matendo ya huruma Geita

9 March 2025, 2:31 pm

Mchungaji wa kanisa la waadventisti Wasabato Geita kati akizungumza na mgonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Geita. Picha na Mrisho Shabani

Jamii imeombwa kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji ikiwemo wagonjwa , wafungwa na wale wanaoshi katika mazingira magumu.

Na Mrisho Shabani:

Kanisa la Waadventisti Wasabato Mtaa wa Geita kati limetoa zawadi nakuwaombea wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Geita mkoani Geita ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya juma la matendo ya huruma kwa kanisa hilo.

Akizungumza baada ya kuwatembelea wagonjwa , kuwaombea nakuwapatia zawadi  mbalimbali leo Machi 09,2025 Mchungaji wa kanisa hilo Babu Sobu Osodo akiwa ameambata na viongozi na waumini wa kanisa hilo amesema utaratibu huo wa kuwakumbuka wahitaji utakuwa endelevu kwakuwa ni agizo la Mungu.

Viongozi na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato Geita kati wakiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Geita kutoa zawadi. Picha na Mrisho Shabani.
Sauti ya Mchungaji Osodo

Aidha mzee wa kanisa hilo George Haiti , Kiongozi wa vijana Charles Pani na muumini wa Teddy Clifordy wameiomba jamii kutochoka kutenda mema ikiwemo kuwasaidia watu wenye mahitaji kwakuwa wapo wengi na wanahitaji kusaidiwa ili kuishi kama watu wengine.

Sauti ya viongozi wa kanisa

Katibu wa afya katika Hospitali ya Manispaa ya Geita Magoma Butaga amelipongeza kanisa hilo kwa kuwakumbuka wagonjwa huku akiwaomba watu wengine kuendelea kujitokeza katika Hospitali hiyo kutoa msaada kwa wahitaji.

Sauti ya katibu wa afya
Viongozi na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato Geita kati wakiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Geita kutoa zawadi. Picha na Mrisho Shabani.