

3 May 2025, 3:30 pm
Mapenzi hayana mwenyewe, lakini wakati mwingine huibua taharuki kwenye Jamii pale wawili wasipofikia makubaliano.
Na: Kale Chongela:
Taharuki yaibuka baada ya msichana ambaye alitambulika kwa jina moja la Eunice, mkazi wa mtaa wa Shilabela na mjasiriamali ambaye anauza mahindi katika soko lilipo eneo hilo kata ta Buhalahala manispaa ya Geita kwa kupokea shilingi 10,000 ya mwanaume na kisha kukiuka makubalino yao.
Bi. Eunice amesema kijana huyo alimpe shilingi Elfu kumi akiwa kwenye kisima wakati anachota maji ndipo kina huyo almfuata na kudodosho shilingi Elfu ndipo mwanamke huyo akaichukua na baada ya siku chake kijana huyo akawa anamtaka kimapenzi ambapo mwanamke huyo alikuwa hataki.
Baadhi ya mashuhuda wameshangazwa na tukio hilo huku wakiwasihi wanawake kuwa waminifu .
Kwa upande wake balozi wa shina namba moja Bi. Rehema Mabina amekiri kuwa watu hao wanaishi katika ubalozi wake ambapo kijana huyo alibeba vyombo vya Yunis kama sehemu ya kujilipa shilingi elfu kumi kwani alishindwa kutoa penzi baada ya kupewa kiasi hicho cha fedha.