Storm FM

Mama avunja nyumba ya mume wake wa zamani

21 April 2021, 11:30 am

Na  Nichoras Paul Lyankando:

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha nyamalulu  katika halmashauri ya wilaya ya Geita amefanya uharibifu wa kubomoa nyumba ya aliekuwa mmewake wa zamani huku ikielezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na Storm FM  Charles Katisho ambae alikuwa mume wa mama huyo amesema mwanamke huyo alikuwa akiishi katika mji mdogo wa katoro mara baada ya kuachana na mmewe amesema yeye hajui chanzo cha mama huyo kufanya uharibifu wa kubomoa nyumba na hii inakuja mara baada ya mzee Katisho kuoa mke mwingine mara baada ya kuachana na mwanamke huyo.

Charles Katisho

Kwa upande wake mmoja wa wanafamilia katika mji huo ambae tukio la kubomolewa kwa  nyumba wakati linatokea alikuwa nyumbani amesema mwanamke huyo alikuwa anatumia silaha aina ya shoka kubomoa  nyumba hiyo lakini walipojaribu kumzuia alitishia kuwajeruhi kwa shoka hilo.

Hata hivyo mara baada ya mama huyo kufanya tukio la kubomoa nyumba aliwatoa ngombe zizini na ndipo wananchi wakakusanyika kumzuia.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho bwana Mathius Bulima ambaye yeye hakuwa tayari kulizungumzia tukio hilo lakini amesema taarifa za tukio hilo zilifika ofisini kwake na mama huyo kupelekwa polisi huku wakiazimia mama huyo kukarabati nyumba alizoharibu kwa gharama zake.