Storm FM

Mchezo wa Geita Gold FC na Kagera Sugar kurudiwa leo, wanaanzia walipoishia

17 September 2023, 1:47 pm

Changamoto ya taa katika viwanja vinavyotumika na vilabu vya Ligi kuu ya NBC ni ya pili kutokea, baada ya ile iliyotokea katika Dimba la Benjamin Mkapa linalotumiwa na vigogo wa soko la Tanzania Simba SC na Yanga SC.

Na Zubeda Handrish- Geita

Mchezo wa Geita Gold FC wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar uliokuwa upigwe full time siku ya jana Septemba 16, 2023 uliahirishwa na kuishia dakika ya 39’ pekee bila ya kufungana kutokana na taa za uwanja wa Kaitaba, Kagera kupata hitilafu.

Hivyo mchezo huo utaendelea leo (Jumapili) ulipoishia jana dakika ya 39’ na utapigwa majira ya saa 10 jioni badala ya jana ulivyopigwa saa 1:00 usiku.