Storm FM

Breaking News: Mtu Mmoja Ajeruhiwa Kutokana Na Ajali Ya Gari.

8 June 2021, 4:06 pm

Na Ester Mabula:

Mtu Mmoja ambae hakujulikana kwa jina Wala Makazi amejeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Hiace lenye namba za usajiri T- 115 – DGV  wakati alipokuwa akijaribu kuvuka Barabara na baiskeli.

Baadhi ya abiria waliyokuwa ndani ya Hiace hiyo wamesema Dereva wa gari hilo alikuwa akijaribu kulipita gari aina ya Costa lenye namba za usajiri T 386 – DCT ambalo lilikuwa likielekea Katoro ndipo mwendesha baiskeli huyo akakatiza Barabara bila kuangalia nakupelekea kugongwa.