Storm FM

Nyumba kuezuliwa serikali mkoani Geita yaingilia kati

20 September 2023, 2:58 pm

Moja ya nyumba iliyoezuliwa na mvua kijiji cha Mnyala Kata ya Nkome Geita. Picha na Mrisho Sadick

Serikali Mkoani Geita imetoa tahadhari kwa watu wenye makazi duni kuhakikisha wanaboresha makazi yao ili kuepuka madhara kutokana na mvua zilizoanza kunyesha nakuleta madhara kwa baadhi ya wananchi.

Na Mrisho Sadick:

Siku chache baada ya Nyumba kadhaa kuezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Mnyala Kata ya Nkome wilayani Geita, serikali mkoani Geita kupitia idara ya maendeleo ya jamii imeanza kutoa elimu kwa wananchi ya ujenzi wa makazi bora ili kukabiliana na changamoto kama hiyo kipindi hiki cha mvua.

Afisa maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Last Lingson amesema wameanza kutoa elimu kwa wananchi hususani vijijini ya kujenga na kuboresha makazi yao ili kukabiliana na changamoto ya mvua na upepo mkali nakwamba katika kipindi cha mwaka 2022/2023 wamepita katika kata 52, vijiji 92 kuhamasisha ujenzi wa makazi bora na katika hamasa hiyo nyumba bora zilizoanza kujengwa nakuboreshwa ni 2,599.

Last Lingson Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Geita akizungumzia kampeni ya ujenzi wa makazi bora. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Afisa Maendeleo

Hivi karibuni mvua iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Mnyala Kata ya Nkome wilayani Geita iliezua baadhi ya nyumba huku wahanga wa tukio hilo wakiioba serikali kuchukua hatua za haraka katika kipindi hiki cha mvua.

Sauti ya wahanga wa tukio