Storm FM

Vyombo vya maamuzi kikwazo mapambano dhidi ya ukatili Geita

12 September 2023, 9:02 pm

Viongozi wa serikali ya Mkoa wa Geita wakiwa katika kikao na naibu Waziri wa maendeleo ya jamii . Picha na Mrisho Sadick

Vitendo vya ukatili bado changamoto kubwa Mkoani Geita huku mzigo huo vikipewa vyombo vya kutoa maamuzi kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Na Mrisho Sadick – Geita

Naibu waziri wa maendeleo ya Jamii , jinsia, Wanawake na makundi maalumu Mwanaidi Ali Khamis amevitaka vyombo vya kutoa maamuzi kuharakisha uchunguzi nakutoa uamuzi wa kesi mbalimbali za vitendo vya ukatili  ili kuepuka kupoteza ushahidi na watuhumiwa kuachiwa huru.

Mhe Mwanaidi Ali Khamis ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa serikali ya Mkoa wa Geita katika ziara yake Mkoani humo ya kufuatilia tathimini ya Utekelezaji wa sera , sheria na miongozo mbalimbali inayotekelezwa na wizara hiyo.

Naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na watendaji wa serikali. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya naibu waziri

Baadhi ya Wananchi Mkoani Geita Ester Robert na John Daud wamesema kutotolewa haraka kwa maamuzi ya kesi za vitendo vya ukatili inawakatisha tamaa.

Sauti ya wananchi

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mwanaid Ali Khamis ametembelea vikundi vya wanawake vya uzalishaji na Uchumi nakusifu jitihada hizo huku akisema serikali itawaunga Mkono katika mapambano hayo.

Sauti ya naibu waziri