Storm FM

Kichanga cha siku 2 chakutwa kimefariki katika dampo la uchafu.

6 January 2023, 10:03 am

Na Kale Chongela:

Katika hali ya kusikitisha  kichanga kilichokadiliwa kuwa na siku mbili  kimekutwa kimefariki dunia katika  dampo la uchafu lililopo katika uwanja wa CCM kalangalala mjini Geita.

Kaimu kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokaji  mkoani Geita Inspekta Edward Lukuba  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  ambapo amesema uchunguzi wa awali imebainika kuwa  mtoto huyo amekutwa akiwa amefariki dunia  na kwamba jitihada za kumtafuta aliyetenda kosa hilo  zinaendelea.

Kwa upande wao baadhi ya mashuhuda wamesema eneo hilo ni kwa ajili ya kutunza taka ngumu lakini katika hali ya kusikitishwa alionekana mwanaume akiwa na mfuko uliokuwa ukionekana kuwa ni taka ngumu na  baada ya kwenda kwenye dampo hilo imeonekana kuwa ni kichanga kimetupwa.