Storm FM

Neema ya maji yawafikia wananchi wa Chabulongo

23 August 2023, 8:19 pm

Chanzo cha maji kilichotengenezwa na Kanisa la TAG

Kukosekana kwa maji katika kijiji cha Chabulongo kumewatia moyo viongozi wa Kanisa la TAG Chabulongo kutoa msaada.

Na Kale Chongela-Geita

Wakazi zaidi ya 360 kunufaika na mradi wa maji katika mta wa Chabulongo, kata ya Bung’hwangoko mradi ambao umefadhiliwa na Shirika la NEEMA kutoka nchini Marekani.

Sauti ya wakazi wa Chabulongo wakizungumzia uwepo wa maji

Akizungumza na Storm FM Mchungaji wa eneo hilo Bi. Ester Nyamizi amesema Hafla hiyo ya uzinduzi wa kisima hicho cha maji kimeambatana na zoezi la ufunguzi wa Kanisa la TAG katika eneo hilo huku akiushukuru uongozi wa ene na kwamba kisima hicho kitawarahisishia wakazi upatikanaji wa maji kwa haraka.

Sauti ya Bi. Ester Nyamizi Mchungaji wa Kanisa la TAG

Mwenyekiti wa Shirika hilo la NEEMA kutoka nchini Marekani Bw. Scott Wiliamu Winters ambaye amefadhili kufanikisha kuwepo kwa maji hayo amesema ni mara baada ya uongozi wa Kanisa hilo kuwasilisha changamoto ya uhaba wa maji safi na salama ndipo wakaanza taratibu ya kuchimba kisima ili wakazi wa eneo hilo waweze kupata maji.

Sauti ya Mwenyekiti wa Shirika hilo la NEEMA kutoka nchini Marekani Bw. Scott Wiliamu Winters na mkalimani wake.