Storm FM

Mkuu wa mkoa wa Geita akagua miradi Nzera.

11 March 2022, 5:38 pm

Na Zubeda Handrish:

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule leo March 10, 2022 amefanya ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ikiwamo ya Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Nzera-Nyanza Kupitia Fedha za Mradi wa Kuboresha Elimu SEQUIP iliyopo katika Kata ya Nzela mtaa wa Nyanza.

Pia amefanya ziara katika Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita linalojengwa katika Kata hiyo, Na mwisho kuangalia maendeleo ya uendelezaji wa utekelezaji wa mpango wa anuani za makazi.