Storm FM

Wahandisi Geita mji watakiwa kusimamia miradi

3 August 2023, 4:28 pm

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Abdala Shaib akizindua Gari la kubeba wagonjwa kituo cha afya Nyankumbu Geita mjini. Picha na Mrisho Sadick

Katika kukabiliana na changamoto ya huduma za afya katika Kata ya Nyankumbu, serikali kupitia Halmashauri ya mji wa Geita imefanya upanuzi kwa kuongeza majengo nakununua Gari la kubebea wagonjwa.

Na Mrisho Sadick:

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib amewataka wahandisi  wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuacha uzembe katika usimamizi wa miradi kwakuwa serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea upanuzi wa Kituo cha Afya Nyankumbu mjini Geita na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa majengo saba nakuzindua Gari la wagonjwa, mradi ambao umeghalimu zaidi ya milioni 700 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Abdala Shaib akiweka Jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Majengo saba kituo cha afya Nyankumbu Geita mjini. Picha na Mrisho Sadick

Sauti ya Abdalla Shaib

Baadhi ya viongozi na wakazi wa Kata ya Nyankumbu akiwemo Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu , Diwani na Kata hiyo Lunyaba Mapesa wameipongeza serikali kwa upanuzi wa kituo hicho kwani Kata hiyo ina idadi kubwa ya watu ambao wanahitaji huduma muhimu kama hiyo.

Sauti ya wananchi na viongozi wa Nyankumbu

Awali akikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati na Nyumba ya Mganga wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 180 katika mtaa wa Shinamwenda, kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru akatoa maelekezo ya kufanyika marekebisho katika dosari zilizobainika wakati wananchi wakiendelea kupatiwa huduma.