Storm FM

Wawili wafariki dunia baada ya kufukiwa na udongo Magenge

7 June 2024, 11:54 am

Shimo katika eneo la Magenge ambapo shughuli za uchimbaji mdogo zinafanyika. Picha na Edga Rwenduru

Uchimbaji mdogo wa madini kwenye maeneo yasiyo rasmi katika baadhi ya maeneo mkoani Geita bado ni kitendawili ambacho kinapelekea changamoto ikiwemo wachimbaji kupoteza maisha kutokana na ubovu wa miundombinu.

Na: Edga Rwendru – Geita

Watu wawili wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na udongo wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa madini katika machimbo yasiyo rasmi  eneo la Magenge wilayani na mkoani Geita.

Baadhi ya wachimbaji wa wadogo wakishiriki zoezi la uokoaji. Picha na Edga Rwenduru

Tukio hilo limetokea Juni 04, 2024 majira ya asubuhi. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Wambura Fide amesema tukio la watu hao kufukiwa na udongo limetokea katika eneo lililokatazwa kuendesha shughuli za uchimbaji kutokana na eneo hilo kutokuwa na usalama.

Sauti ya afisa wa zimamoto
Afisa wa zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Wambura Fide. Picha na Edga Rwenduru

Mwenyekiti wa kijiji Mathias Deo na diwani wa kata hiyo Edward Misungwi wameeleza kuwa wamiliki wa leseni za uchimbaji wa madini wanatakiwa kubainisha maeneo ya kufanyia kazi kwani uongozi ulikuwa hauna taarifa kuwa eneo hilo limekatazwa na haukuwa na taarifa kama eneo hilo kuna mmiliki mwenye leseni ya utafiti.

Sauti ya mwenyekiti na diwani

Kwa upande wake Abdul Joseph Stanslausi ambaye ni Mmiliki wa leseni hiyo amesema kabla ya kutokea kwa ajali hiyo alikuwa ametoa taarifa kwa viongozi husika.

Sauti ya mmiliki wa leseni