Storm FM

Shule za Msingi Geita zatakiwa kufanya mijadala

25 April 2021, 2:27 pm

Walimu shule za msingi  katika halmashauri ya mji wa Geita wameshauriwa kuandaa mijadala shuleni baina ya shule jirani ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa kujieleza kitaaluma .

Ushauri huo umetolewa na Afisa tawala Wilaya ya  Geita  Bw Inocent Mabiki  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika  mjadala  uliofanyika katika kata ya Nyankumbu  na kuzikutanisha shule 6 kwa lengo la kushindana kwa hoja na kupanuaulewa kwa wanafunzi.

Afisa tarafa mji wa Geita

Mdahalo huo ulikuwa unahusu  uzalendo kwa watanzania na  shule ya msingi Mbugani imeibuka mshindi kwa 90% dhidi ya shule ya msingi Nyankumbu iliyopata 80% na wanafunzi wa shule zote shiriki kusema kuwa  k suala hili likizingatiwa  na kutiliwa mkazo litawasaidia wanafunzi kuendelea kufanya vizuri.

Kwa upande wake afisa utamaduni halmashauri ya mjii wa Geita  Bi Ngianasia Kisamo  amesema watahakikisha wanasimamaia zoezi hilo liwe endelevu katika halmashauri zote ili na kufanyika kwa mujibu wa taratibu za TAMISEMI.