Storm FM

Mwanafunzi afariki wakati akiogelea bwawani Geita

6 February 2024, 4:48 pm

Bwawa lililosababisha kifo cha Mwanafunzi Mbabani. Picha na Kale Chongela

Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha mashimo makubwa kujaa maji nakuleta madhara kwa watu na wanyama waliyopembezoni mwa mashimo hayo.

Na Kale Chongela:

Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mbabani Kata ya Mtakuja Halmashauri ya mji wa Geita  wilayani Geita amefariki dunia wakati akiogelea kwenye bwawa baada ya maji kumzidi.

Tukio hilo limetokea majira ya saa kumi jioni siku ya jumapili februari 4,2024 katika bwawa lililopo katika mtaa huo ambalo limechimbwa zaidi ya miaka saba iliyopita kwa matumizi ya ujenzi wa barabara huku wakazi wa mtaa huo wakiiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa mashimo yaliyochimbwa kwa shughuli mbalimbali kwani yamejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Sati ya wakazi wa Mbabani

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo Daud Zwahayo amesema wananchi kwa kushirikiana na ofisi yake walifanya jitihada za kumuokoa mtoto akiwa ziligonga mwamba kutokana na taarifa za tukio hilo kuchelewa kufika kwa jeshi la zimamoto na uokoaji.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbabani
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Hamis Dawa. Picha na Kale Chongela

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji  Mkoani Geita Hamisi   Dawa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni msichana mwenye umri wa miaka 13 Domitila Masumbuko huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua.

Sauti ya Kamanda Zimamoto