Storm FM

Taharuki mlipuko na maporomoko ya tope Chato

2 February 2024, 4:12 pm

Hali ilivyo kwa baadhi ya maeneo ya kitongoji cha Iloganzila baada ya maporomoko ya tope. Picha na Mrisho Shabani

Siku chache baada ya kutokea kwa maporomoko makubwa ya tope mkoani Manyara hali hiyo imejitokeza Chato mkoani Geita japo siyo kwa ukubwa.

Na Mrisho Shabani

Wakazi wa kitongoji cha Iloganzara kijiji cha Songambele wilayani Chato Mkoani Geita wamekumbwa na taharuki baada ya kutokea kwa mlipuko wa tope lililoambata na maji nakuharibu mazao ya chakula , mifugo na makazi ya watu.

Tukio hilo limetokea Januari 30 mwaka huu majira ya saa 12 jioni huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo Frola Benjamine na Magesa Ngereja wakisema walianza kuona kama mvuke wa moshi kutoka mlimani uliyokuwa ukirusha tope juu hali iliyosababisha tope hilo kuanza kwenda kwenye makazi ya watu huku liking’oa miti, kuharibu mazao ya chakula nakusomba baadhi ya mifugo.

Kamati ya usalama ya wilaya ya Chato wakiwa kwenye eneo lililoathiriwa na tope. Picha na Mrisho Shabani.
Sauti ya Wananchi Chato

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Songambele Fikiri Musela amesema eneo hilo kipindi cha nyuma lilikuwa na shughuli za uchimbaji wa madini huku diwani wa kata ya iparamasa kilipo kijiji hicho Faustine Mbasa  ameiomba serikali kufanya uchunguzi zaidi ili kuondoa hofu kwa wananchi.

Sauti ya Mwenyekiti na Diwani

Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdedith Katwale amefika eneo la tukio huku akiiomba taasisi ya jiolojia na utafiti wa madini GST kuhakikisha inafanya uchunguzi haraka kubaini changamoto ya mlipuko huo huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kuwa wavumilivu huku mjiolojia mkuu kutoka taasisi ya GST John Kalimenze amezungumzia tukio hilo.

Sauti ya DC na Mjiolojia GST