Storm FM

Wanaume watakiwa kujitokeza kufanyiwa tohara Geita

28 May 2021, 2:10 pm

Wanaume ambao hawajafanyiwa tohara Mkoani Geita wameshauriwa kujitokeza katika vituo vya afya kupatiwa huduma hiyo kwani inasaidia kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo kupunguza 60% ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Rai  hiyo imetolewa na Mratibu wa kuthibiti  Ukimwi Mkoani Geita  Dkt Furaha  Kibaba  wakati akizungumza na Storm FM Ofisini kwake ambapo amesema mwitikio wa wanaume kujitokeza kupata huduma hiyo mkoani Geita ni mzuri na kuwashauri ambao bado wafike katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo kwani huduma hiyo inatolewa bure.

Mratibu wa Ukimwi

Katika Hatua Nyingine  Dkt Kibaba ameongeza kwa kusema  kuwa kwa mujibu wa Takwimu za wanaume kufanyiwa tohara mkoani Geita mwaka 2020 kwa kuanzia mwezi januari hadi disemba zinaonesha kuwa wanaume Elfu 47,488 katika mkoa mzima wa Geita walifanyiwa tohara.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi  Mkoa wa Geita wamesema  licha ya huduma hii kutolewa bure bado shughuli za utafutaji mali  zinawafanya kushindwa  kutimiza adhima hiyo.