Storm FM

CHAMIJATA yaja na mikakati kuenzi tamaduni

19 July 2023, 6:23 pm

Wanachana wa CHAMIJATA katika kikao. Picha na Kale Chongela

Inadaiwa kuwa utandawazi ni moja ya njia inayopelekea mila na desturi za kiafrika kusahaulika, na watu wa tamaduni hizo kufuata mambo ya kigeni, hilo limewainua CHAMIJATA kusimama kidete katika kuzilinda tamaduni hizo.

Na Kale Chongela- Geita

Katika kuendelea kuboresha utamaduni wa Tanzania Chama cha Michezo ya Jadi Tanzaznia CHAMIJATA  mkoa wa Geita kimekuja na mikakati ya namna ya kuhakikisha wanaenzi tamaduni za kiafrika.

Mwenyekiti wa CHAMIJATA Bw. Dunia Mrisho Mlea baada ya kikao kilichofanyika leo Julai 19, 2023 katika ofisi ya kata ya Nyankumbu Mjini Geita, amesema mikakati ni kuhakikisha jamii inaishi katika misingi inayokubalika na si kwenda tofauti na maadili ya watanzania.

Sauti ya Mwenyekiti wa CHAMIJATA Bw. Dunia Mrisho Mlea
Diwani wa kata ya Nyankumbu Bw. John Lunyaba Mapesa. Picha na Kale Chongela

Diwani wa kata ya Nyankumbu Bw. John Lunyaba Mapesa ambaye ameshiriki kwenye kikao hicho na wanachama hao ametumia fursa hiyo kuwashauri kuwa na desturi ya kutembelea shule zote za msingi na sekondari kwa lengo la kutoa elimu juu ya kuenzi maadili ya kitanzania.

Sauti ya Diwani wa kata ya Nyankumbu Bw. John Lunyaba Mapesa