Storm FM

Naibu waziri wa Habari atoa maagizo kwa wakandarasi nchini

10 January 2024, 6:57 pm

Naibu waziri wa Habari aliyevaa miwani akiwa katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilayani ya Chato alipowasili kwa ajili ya ziara ya kikazi. Picha na Mrisho Sadick

Serikali ya awamu ya sita imejidhatiti katika kuimarisha mawasiliano nchini kwa kuongeza kasi ya ujenzi wa minara na vituo vya kuongeza nguvu ya mawasiliano.

Na Mrisho Sadick – Chato

Naibu Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandis Kundo Methew amewaagiza wakandarasi wote nchini wanaotekeleza ujenzi wa minara ya mawasilino 758 na vituo vya kuongeza nguvu ya mawasiliano kuhakikisha kufikia mwanzoni mwa mwaka 2025 kila mkandarasi awe amekabidhi mradi.

Mhandis Kundo ametoa maagizo hayo baada ya kukagua kituo cha kuongeza nguvu ya mawasiliano wilayani chato Mkoani Geita kinachojengwa kwa thamani ya bilioni 1.8 huku akisema serikali imejipambanua kuhakikisha inaboresha mkongo wa taifa kwa kutoa magari 45 yenye thamani ya bilioni 7.28 kwa ajili ya kuimarisha mkongo huo.

Sauti ya Naibu Waziri wa Habari
Naibu Waziri wa Habari akikagua kituo cha kuongeza nguvu ya mawasiliano wilayani Chato.Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandisi Deusdedith Katwale amepongeza hatua hiyo huku akiiomba wizara hiyo kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano kwenye hifadhi za taifa zilizopo katika eneo hilo za Rubondo na Burigi Chato.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Chato
Naibu Waziri wa Habari akikagua kituo cha kuongeza nguvu ya mawasiliano wilayani Chato. Picha na Mrisho Sadick

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Meneja wa TTCL Mkoa wa Kagera ambao unahudumia wilaya ya Chato Theopister Mark amesema mradi huo unalengo la kupanua huduma  nakuongeza kasi ya mawasiliano huku diwani wa Kata ya Chato ulipo mradi huo Mange Ludomya akiipongeza serikali kwa hatua hiyo.

Sauti ya Meneja wa TTCL Kagera na Diwani Chato