Storm FM

Wananchi wahofia kuporwa ardhi yao na kijiji

17 August 2023, 11:57 am

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Salagulwa wanaolalamikia kutaka kupokonywa ardhi yao. Picha na Mrisho Sadick

Migogoro ya ardhi kwa baadhi ya maeneo wilayani Geita imekuwa mwiba mchungu kwa wananchi hususani vijijini kwakuwa wengi wao hawajui waende wapi wakapate haki zao.

Na Mrisho Sadick:

Wakulima wa kijiji cha Salagulwa Kata ya Nyamlolelwa wilayani Geita wameiomba serikali kuingilia kati sakata la uongozi wa kata hiyo kutaka kuwanyan’ganya ardhi yao ya makazi na mashamba kwa madai kuwa eneo hilo ni tengefu kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.

Wananchi hao wamesema kupitia mkutano wa kijiji viongozi wa kata hiyo wamewataka wananchi hao kuondoka katika eneo hilo wakieleza kuwa ni agizo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Geita kuwa eneo hilo ni tengefu kwa ajili ya shughuli za uwekezaji jambo ambalo limezua hofu kwa wananchi hao.

Sauti ya wananchi wa Salagulwa

Francis Isaya aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji hicho anaedaiwa kufukuzwa na viongozi wa kata ya Nyamlolelwa anasema alikuwa anawatetea wananchi wake wasiondolewe katika eneo hilo akaambulia kuvuliwa wadhifa huo.

Sauti ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Salagulwa
Makazi ya wananchi ambayo yametakiwa kuondolewa katika eneo hili kwa madai kuwa ni eneo la uwekezaji. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe akizungumza kwa njia ya simu amekanusha ofisi yake kutoa maagizo ya kufukuzwa kwa wananchi nakuwata kuwa wavumilivu wakati suala hilo akiendelea kulifanyia kazi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita