Storm FM

Geita Gold FC yaanza kusuka kikosi

15 July 2023, 5:32 pm

Mchezaji wa Geita Gold FC Elias Maguli. Picha na Geita Gold FC

Leo ni siku ya 15 tangu kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili ambapo Julai 1, 2023 rasmi vilabu katika ngazi mbalimbali za ligi ziliruhusiwa kuongeza wachezaji kwaajili ya msimu mpya wa 2023/24.

Na Zubeda Handrish- Geita

Klabu ya Geita Gold FC yenye maskani yake hapa mkoani Geita, imemuongeza mkataba wa mwaka mmoja mchezaji wake Elias Maguli hadi 2024.

Kupitia kwa Afisa habari wa klabu hiyo Samwel Dida ameweka wazi wachezaji walioachana nao kwa kumaliza mkataba na aliyevunja mkataba.

1.Dan Lyanga
2.George Wawa
3.Marc Arakaza
4.Jofrey Manyac
5.Jonathan Ulaya
6.Mussa Gadi
7.Shinobu Sakai
8.Jonathan Mwaibindi
9.Juma Luizio (kaomba kuvunja mkataba).