Storm FM

Wananchi wazima jaribio la wizi wa nyaya za umeme

6 July 2023, 6:21 pm

Wananchi wa kijiji cha Kaduda wakiwa eneo la tukio. Picha na Mrisho Sadick

Kundi la watu zaidi ya 20 limefurushwa kwa madai ya kutaka kuiba nyaya za umeme zilizokuwa zimehifadhiwa katika shule ya sekondari.

Na Mrisho Sadick:

Wakazi wa kijiji cha Kaduda Kata ya Katoro wilayani Geita wamezima jaribio la wizi wa nyaya za umeme za Kampuni binafsi ya kuunganisha umeme vijijini ya SINO TECK LTD zenye thamani ya shilingi milioni 12 zilizokuwa zimehifadhiwa katika shule ya sekondari kaduda kwa ajili ya kuwasambazia umeme wakazi wa kijiji hicho.

Wananchi hao wamesema walibaini viashiria vya wizi wa nyaya hizo kutoka kwa kundi la watu zaidi ya ishirini waliyofika katika kijiji hicho wakiwa na Gari aina ya Canter yenye namba za usajili T 121 DMG usiku wa manane ndipo wakaweka mtego nakuwafurusha watu hao nakubaki na gari lao.

Sauti ya wakazi wa kijiji cha Kaduda

Baada ya wananchi kufanya upekuzi kwenye gari hilo wamekuta nyaraka mbalimbali ikiwemo kadi ya gari , lesseni ya udereva na kadi za Benki huku diwani wa kata hiyo akisisitiza wahusika watafutwe na wachukuliwe hatua.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Katoro Kigongo Sweya
Kaimu kamanda wa Polisi Geita ACP Berthaneema Mlya. Picha na Mrisho Sadick

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita kamishna msaidizi wa Polisi  ACP Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakwamba uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.