Storm FM

Ni Yanga SC au Azam FC kutinga fainali leo?

9 August 2023, 3:20 pm

Mashabiki wa soka Nyankumbu, Geita. Picha na Zubeda Handrish

Darby ya Dar es salaam imeibua hisia za mashabiki wa soka mkoani Geita, na kufunguka timu yenye nafasi zaidi ya kutinga fainali ya Ngao ya Jamii kati ya michezo ya leo.

Na Zubeda Handrish- Geita

Michuano ya Ngao ya Jamii Tanzania inaanza kutimua vumbi leo Agosti 9, 2023 kwa mchezo mmoja wa nusu fainali kati ya Young Africans SC dhidi ya Azam FC utakaopigwa katika dimba la Mkwakwani Tanga majira ya saa 1:00 jioni.

Mashabiki wa soka mjini Geita wamefunguka juu ya ugumu na wepesi wa mechi ya kwanza ya leo Agosti 9, 2023 ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC.

Sauti ya Mashabiki wa soka Nyankumbu, Geita

Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 1:00 usiku, katika Dimba la Mkwakwani, Tanga.

Shabiki wa soka Nyankumbu, Geita. Picha na Zubeda Handrish

Kuelekea mchezo huo, Yanga itamkosa winga wake Jesus Moloko ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu huku Azam FC ikimkosa kiungo wake mpya Yannick Bangala ambaye ana jeraha la goti.

MECHI 5 ZA MWISHO YANGA vs AZAM
• Yanga SC 1-0 Azam FC
• Azam FC 2-3 Yanga SC
• Yanga SC 2-2 Azam FC
• Azam FC 1-2 Yanga SC
• Yanga SC 2-0 Azam FC