Storm FM

Geita queens yavuna alama 1 ligi ya wanawake

30 April 2024, 6:04 pm

Goli kipa wa Geita queens (jezi nyeusi) ulingoni. Picha na Juma Zacharia

Ikiwa ni mwendelezo wa Ligi kuu ya wanawake Tanzania bara, Geita queens yaonesha matumaini kwa kupata sare.

Na: Juma Zacharia – Geita

Kikosi cha Geita Gold Queens kutoka mkoani Geita kimeendelea kukosa ushindi katika mwendelezo wa ligi kuu wanawake Tanzania bara.

Kikosi hicho kimeshuka dimbani April 29 kucheza na Baobab queens kutoka Dodoma na kuondoka na alama 1 baada ya sare ya goli 1-1 mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya wasichana Nyankumbu uliopo Geita mjini.

Baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo, kocha wa Geita queens Jullius Richard amesema wamejitahidi kutafuta alama 3 lakini wanaipongeza Baobab queens ilivyocheza huku akiamini bado timu hiyo itasalia ligi kuu.

Sauti ya kocha wa Geita queens

Teddy Thomas mchezaji wa Geita queens akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema ulikuwa mchezo mgumu na mwalimu aliwasisitiza kushambulia zaidi

Sauti ya mchezaji Geita queens

Kwa upande wa Baobab queens, kocha mkuu Paul Domician amesema wamecheza na timu nzuri sababu Geita queens  ipo nafasi za chini katika msimamo hivyo inaleta ushindani.

Sauti ya kocha wa Baobab queens

Naye nyota na nahodha wa Baobab queens, Zuhura Khamis baada ya kuvuna alama moja amesema ulikuwa mchezo mzuri lakini hawakutumia nafasi walizozipata

Sauti ya nahodha wa Baobab queens