Storm FM

Wilaya ya Geita kufanya msako wa wazazi waliotelekeza familia

12 October 2023, 11:05 am

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wilayani Geita wakiwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani mjini Geita. Picha na Mrisho Sadick

Wakati serikali ikiendelea kupambania haki sawa kwa mtoto wa kike wananchi na wadau wametakiwa kuiunga mkono katika mapambano hayo.

Na Mrisho Sadick:

Watendaji wa Mitaa na Kata wilayani Geita wameagizwa kufanya msako nakuwachukulia hatua kali wazazi na walezi ambao wamewatelekezea familia watoto wao nakuwakosesha haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Geita katika  maadhimisho ya siku ya Mtoto wa kike duniani katika viwanja vya shule ya Sekondari Nyanza wilayani Geita.

Sauti ya afisa elimu Halmashauri ya mji wa Geita
Margaret Macha Afisa elimu Halmashauri ya mji wa Geita akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto kike duniani mjini Geita . Picha na Mrisho Sadick.

Kwa upande wake msimamizi wa masuala ya jinsia katika mradi wa KAGIS kutoka shirika la Plant Internation Hildegada Mashauri amesema kwasasa jamii imeendelea kuwa na mwamko hususani katika kumsomesha mtoto wa kike kwani hapo awali hali hayo haikuwepo kabisa.

Sauti ya msimamizi masuala ya jinsia mradi wa KAGIS

Maadhimisho hayo yameratibiwa na Shirika la Plan International kwa kushirikiana na Rafiki SDO kupitia mradi wa KAGIS unaofadhiliwa na serikali ya watu wa Canada huku wanafunzi na wadau wa kutetea haki za Mtoto wa kike wakisema.