Storm FM
Storm FM
22 July 2026, 8:56 am

Ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari utasaidia kupunguza changamoto kwa watoto wa kike ikiwemo mimba za utotoni wilani Chato
Na Mrisho Sadick:
Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini Paschal Lutandula amemuomba Waziri wa Madini Antony Mavunde kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika sekta za madini, elimu na maji.
Lutandula amesema kuwa licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali bado kuna maeneo yanayohitaji msukumo zaidi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kunufaika ipasavyo na rasilimali zilizopo.
Ombi hilo amelitoa wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Mavunde wilayani Chato ambapo alifika kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Waziri Mavunde ambaye pia ni mlezi wa shughuli za maendeleo Mkoa wa Geita Mhe Antony Mavunde ameahidi kuyafanyia kazi maeneo yaliyobainishwa kwa kushirikiana na wizara husika na viongozi wa mkoa ili kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi kwa manufaa ya wananchi.