Storm FM
Storm FM
3 September 2026, 6:49 pm

Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na mawasiliano TPDC akitoa elimu kwa waandishi wa habari waliohudhuria semina. Picha na Ashura Ramadhani
TPDC inaendelea kutekeleza majukumu yake katika kuhakikisha rasilimali za mafuta na gesi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Na: Ashura Ramadhani
Waandishi wa habari mkoani Geita wamehudhuria semina maalum inayolenga kuwajengea uelewa kuhusu shughuli na mipango ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, matumizi ya gesi asilia pamoja na maendeleo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, EACOP.
Akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika Septemba 3 2026 katika ukumbi wa Harvest Hotel Geita mjini, Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na mawasiliano TPDC Marie Msellemu ameeleza mipango mbalimbali ya shirika, akisisitiza kuwa TPDC inaendelea kutekeleza majukumu yake katika kuhakikisha rasilimali za mafuta na gesi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Sauti ya mkuu wa kitengo cha uhusiano na mawasiliano TPDC
Aidha, semina hiyo imeangazia pia maendeleo na umuhimu wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki – EACOP, unaohusisha Tanzania na Uganda ambapo Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP kutoka TPDC Jumanne Mohammed Said ametoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi huo, hatua zilizofikiwa pamoja na umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania na eneo la Afrika Mashariki.
Sauti ya kaimu mratibu wa mradi wa EACOP kutoka TPDC
Akizungumza kwa niaba ya waandishi waliohudhuria semina hiyo Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Geita Renatus Masuguliko, amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kupata taarifa sahihi ili kuwaelimisha wananchi kuhusu fursa na manufaa yanayotokana na sekta ya mafuta na gesi.
Sauti ya mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Geita

Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria semina hiyo. Picha na Ashura Ramadhani
Semina hiyo imehitimishwa kwa msisitizo wa umuhimu wa ushirikiano kati ya TPDC na vyombo vya habari katika kutoa elimu kwa umma kuhusu sekta ya mafuta na gesi, pamoja na fursa na manufaa yanayotokana na rasilimali hizo.