Storm FM

Twist Elite Football Academy yazinduliwa rasmi ili kukuza vipaji Geita

20 June 2026, 6:55 pm

Mkurugenzi wa Twist Elite Football Academy Ally Twist akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho. Picha na Ester Mabula

Kituo hicho kitakuwa kikiendesha shughuli zake katika viwanja vya shule ya sekondari ya Waja boys iliyopo halmashauri ya manispaa ya Geita chini ya kocha Choki Abeid pamoja na makocha wengine wenye uzoefu wa kuibua vipaji vya watoto.

Na: Ester Mabula

Kituo cha Twist Elite Football Academy kimefunguliwa rasmi leo Juni 20, 2026 kwaajili ya kutoa mafunzo ya mpira wa miguu kwa watoto wadogo kuanzia umiri wa miaka minne hadi 15.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho Mkurugenzi wa Twist Elite Football Academy Ndg. Ally Twist ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Geita (GEDFA) amesema dhamira ya kituo hicho ni kuendeleza vipaji vya watoto na kuwalea katika misingi bora.

Sauti ya mkurugenzi wa Twist Elite Football Academy Ally Twist
Mgeni rasmi katika uzinduzi, Juliana Kimaro ambaye ni Afisa michezo manispaa ya Geita akizungumza. Picha na Ester Mabula

Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi huo Bi. Juliana Kimaro, Afisa michezo halmashauri ya manispaa ya Geita amempongeza mkurugenzi kwa kuanzisha kituo hicho huku akitowa wito kwa wazazi kuchangamkia furasa hiyo ili kuwatengenezea watoto wao msingi mzuri wa maisha ya bàadae.

Sauti ya mgeni rasmi Juliana Kimaro

Baadhi ya wazazi na walezi waliopeleka watoto wao katika kituo hicho wamepongeza hatua hiyo na kueleza itawasidia katika kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto wao.

Sauti ya wazazi na walezi
Watoto waliojiunga na Twist Elite Football Academy wakiendelea na mazoezi mbalimbali. Picha na Ester Mabula