Storm FM

Kata nne kunufaika na milioni 600 kutoka mgodi wa Bucreef Geita

12 December 2025, 12:12

Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita akisaini makubaliano ya utekelezaji wa miradi kupitia fedha za CSR na Mgodi wa Bucreef. Picha na Mrisho Sadick

Vipaumbele vikubwa vya fedha hizo za CSR ni huduma za Afya kwakuwa kata hizo zina ongezeko kubwa la watu kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini.

Na Mrisho Sadick:

Wakazi wa Kata nne za Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wanatarajia kunufaika na fedha za CSR zaidi ya milioni 600 kutoka mgodi wa dhahabu wa Bucreef unaofanya shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo.

Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wananchi kutoka Kata za Lwamgasa , Kaseme , Busanda na Butundwe wanaotarajia kunufaika na fedha hizo katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutokana na fedha hizo na mgodi wa Bucreef , zoezi ambalo limeshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela wamesema fedha hizo zitakuwa chachu ya maendeleo.

Viongozi na wananchi wametembelea sehemu ya mgodi wa Bucreef. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya wakazi Lwamgasa

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bucreef  Isack Bisansaba amesema vipaumbele vikubwa vya fedha hizo za CSR ni huduma za Afya kwakuwa kata hizo zina ongezeko kubwa la watu kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu huku mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba akiahidi kuendelea kuwalinda wawekezaji kwakuwa wamekuwa chachu ya maendeleo.

Sauti ya Meneja Bucreef na Mkuu wa wilaya ya Geita
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano ya CSR. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameupongeza Mgodi huo kwa kuendelea kutekeleza miradi ya huduma za Jamii bila changamoto huku akiwataka watendaji wa serikali na Wananchi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha fedha hizo zinawanufaisha.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Geita