Storm FM
Storm FM
10 October 2025, 05:37

“Chacha ni Nzagamba lililoshiba, liko tayari kwaajili ya kuleta maendeleo katika jimbo la Geita mjini na kuendeleza kutekeleza ilani ya CCM” – Chacha Wambura
Na: Ester Mabula
Katika mwendelezo wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Geita mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhandisi Chacha Mwita Wambura, Oktoba 09, 2025 ilikuwa zamu ya kata ya Nyankumbu.

Akizungumza na wakazi wa kata hiyo na wananchi waliojitokeza kumsikiliza, ameeleza kuwa dhamira yake kuu ni kuleta maendeleo katika jimbo la Geita sambamba na kutatua changamoto ya miundombinu ambayo imekuwa kikwazo katika kata hiyo.

Naye mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM Paschal Sukambi ameeleza kuwa iwapo wananchi watamchagua atahakikisha anapambana kupunguza ajali katika barabara kuu ya kata hiyo ambayo imekuwa kikwazo na chanzo kikuu cha ajali.

Mgeni rasmi katika mkutano huo Nicholaus Kasendamila ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita amesema chama cha mapinduzi kimeendelea kujinasibu kwa kuleta maendeleo na kuwasihi wananchi kuchagua viongozi wa CCM.

