Storm FM

RC Geita akagua mradi wa maji wa bilioni 1 Mbogwe

19 June 2026, 2:26 pm

Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoka kwenye ukaguzi wa mradi wa maji juu ya mlima lilikojengwa tanki la maji. Picha na Mrisho Sadick

Katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama vijijini serikali imeendelea kuchukua hatua za haraka kutekeleza miradi itakayokwenda kuondoa changamoto hiyo.

Na Mrisho Sadick:

Wananchi zaidi ya 12,000 wa Kata za Ilolangulu na Ngemo wilayani Mbogwe mkoani Geita wanatarajia kunufaika na mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni moja unaotekelezwa na Serikali ambao kwa sasa umefikia asilimia 60 ya utekelezaji.

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mbogwe Judith Mudende amesema hayo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela aliyefanya ziara ya kukagua utekelezaji wake.

Tenki la maji lwenye ujazo wa lita elfu 75 litakalo hudumia wakazi wa kijiji cha Ilolangulu. Picha na Mrisho Sadick

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema Serikali imejipanga kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma ya maji safi na salama huku akiahidi kutatua changamoto zinazokwamisha utekelezaji wake.

Baadhi ya wakazi wa kata hizo wameeleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa ya mradi huo nakwamba  utakapokamilika utawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Ripoti ya stori hii na Mrisho Sadick
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza na wananchi wilayani Mbogwe baada ya ukaguzi wa mradi wa maji. Picha na Mrisho Sadick