Storm FM
Storm FM
14 May 2026, 2:57 pm

Mlango wa chuma ulioibiwa na Bededictor.Picha na Kale Chongela
Mkazi wa shilabela mwenyeji wa Mkoa wa Mwanza amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mlango wa chuma unaokadiliwa kuwa na Thamani ya Shilingi Laki mbili.
Na: Kale Chongela
Serikali ya mtaa wa Shilabela kata ya Buhalahala manispaa ya Geita imemkamata Bw Benedictor Bahati mkazi wa shilabela mwenyeji wa Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za wizi wa mlango wa chuma unaokadiliwa kuwa na Thamani ya Shilingi Laki mbili.
Akizungumza na Storm Fm akiwa ofisini kwake Mwenyekiti wa mtaa wa shilabela Bw Fredrick Masalu amesema mtuhumiwa alikamatwa baada ya wananchi kutoa taarifa zinazodai kuwa alionekana akiwa na mlango huo katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika taratibu za kutafuta mteja .
Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa shilabela
Aidha baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtuhumiwa huyo alionekana katika egesho la maafisa usafirishaji akiwataarifu kuwa anauza mlango suala ambalo liliwapa wasiwasi hali iliyopelekea kutoa taarifa katika ofisi ya mtaa huo .
Sauti ya mashuhuda wa tukio hilo

Mtuhumiwa wa wizi wa mlango wa chuma Bw Benedictor Bahati. Picha na Kale Chongela