Storm FM

Geita MC, GGML yapongezwa kufanikisha Tamasha la utamaduni na nyamachoma

23 May 2026, 4:35 pm

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela, mgeni rasmi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha. Picha na Ester Mabula

Tamasha la utamaduni na nyamachoma litakuwa likifanyika kila mwezi ili kuenzi mila na desturi sambamba na kutoa fursa kwa wajasiriamali kujiongezea kipato.

Na: Ester Mabula

Uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Geita kwa kushirikiana nakampuni ya  Geita Gold Minning Limited (GGML) umeandaaa tmasha la utamaduni na nyamachoma ambalo limewakutanisha wakazi wa Geita na maeneo ya kanda ya ziwa kujifunza mila na desturi mbalimbali kupita ngoma za asili, vyakula vya asili na mitindo ya maisha.

Akizungumza Mei 22, 2026 wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo Mkurugenzi wa manispaa ya Geita Yefred Myenzi amesema lengo la tamasha hilo ni kuenzi na kuendeleza mila na desturi sambamba na kutoa fursa kwa wajasiriamali.

Sauti ya mkurugenzi manispaa ya Geita, Yefred Myenzi
Mkurugenzi manispaa ya Geita Yefred Myenzi akitoa taarifa fupi ya maandalizi ya Tamasha la utamaduni. Picha na Ester Mabula

Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti anayesimamia shughuli za uendelevu na mahusiano ya Kampuni barani  Afrika Ndg. Simon Shayo amesema kampuni hiyo inaenzi umoja na ushirikiano kutokana na kufanya kazi na watu wa mataifa mbalimbali.

Sauti ya makamu wa Rais AngloGold Ashanti Simon Shayo
Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti Simon Shayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la utamadnuni. Picha na Ester Mabula

Akizungumza mgeni Rasmi Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela ameipongeza kampuni ya GGML pamoja na viongozi wa manispaa ya Geita kwa kufanikisha tamasha hilo akieleza kuwa tamasha hilo ni mwendelezo wa  kuutangaza mkoa wa Geita.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela
Shughuli mbalimbali za uchomaji nyama zikiendelea katika Tamasha la Utamaduni linalofanyika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu. Picha na Ester Mabula