

9 April 2025, 12:05 pm
Baada ya mafunzo kwa watendaji wa serikali za mitaa, kata, vijiji, wenyeviti na maofisa tarafa, Kamanda wa polisi mkoa wa Geita ameeleza waandishi wa habari juu ya mikakati ya kuondoa watoto wanaoishi mitaani mkoani Geita.
Na: Ester Mabula:
Jeshi la polisi mkoani Geita kwa kipindi cha mwezi machi mwaka huu limefanikiwa kuwakamata watoto 19 wanaoishi mitaani na kufanya utaratibu wa kuwarejesha majumbani kwao.
Taarifa hiyo imetolewa April 08, 2025 na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita SACP Safia Jongo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa semina inayofadhiliwa na Kampuni ya GGML iliyowakutanisha viongozi wa serikali za mitaa, walimu, viongozi wa dini pamoja na Jeshi la polisi kwa lengo la kutoa elimu ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu kupitia program maalumu ya ‘Community Policing Outreach”
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo Mwenyekiti wa mtaa wa Mkoani Salvatory Daniel amelishukuru Jeshi la polisi kwa elimu hiyo huku akiiomba serikali kufanya utaratibu wa kujenga kituo kwaajili ya watoto wanaoishi mazingira magumu.
Elimu hii itafikia makundi ya watu mbalimbali katika Jamii na ilizinduliwa Aprili 04, 2025 na itafanyika kwa muda wa wiki mbili.