Storm FM

Umoja wa madereva bajaji mji wa Katoro wakutana

25 April 2024, 10:04 am

Baadhi ya madereva bajaji katika mkutano wa pamoja baina yao na wadau wa usafirishaji uliofanyika katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro. Picha na Evance Mlyakado

Usafiri wa pikipiki zenye magurudumu matatu maarufu bajaji nchini umekuwa ukitegemewa na wananchi kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya maeneo nchini huku baadhi ya vijana wakijiajiri na kuweza kuendesha maisha yao.

Na Evance Mlyakado – Geita

Umoja wa waendesha bajaji ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Katoro umeitisha mkutano wake na wadau mbalimbali katika sekta hiyo ya usafirishaji lengo ikiwa ni kujadili mambo muhimu yanayoukabili umoja huo.

Katika mkutano huo changamoto mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo madereva bajaji kubeba abiria juu ya kiwango ambacho kinatakiwa pamoja na ukosefu wa leseni kwa madereva jambo ambali linachangia kuongeza ajali za barabarani.

Sauti za baadhi ya madereva bajaji walioshiriki katika mkutano
Baadhi ya madereva bajaji katika mkutano wa pamoja baina yao na wadau wa usafirishaji uliofanyika katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro. Picha na Evance Mlyakado

Katika mkutano huo wadau mbalimbali wa usafirishaji wakiwemo mamlaka ya usafirishaji ardhini nchini LATRA, Jeshi la polisi na viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita walihudhuria na kutoa elimu kuhusu usafirishaji kama anavyoeleza afisa mfawidhi kutoka LATRA Bw. Rajab Suleiman

Sauti ya afisa mfawidhi kutoka LATRA

Kwa Upande wake mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashimu A. Komba amewaasa waendesha bajaji wote ambao hawajajiunga na umoja huo kujiunga huku akiwataka viongozi kuwasaidia vijana hao katika utatuzi wa changamoto zao.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim A. Komba akizungumza katika mkutano wa umoja wa madereva bajaji katika mji wa Katoro. Picha na Evance Mlyakado.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Geita

Katika hatua nyingine DC Komba amewashauri kuzingatia suala la bima za Afya ili ziweze kuwasaidia pindi wanapopitia changamoto ikiwemo kupata ajali

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Geita