Storm FM

TAS yatoa tamko baada ya mtoto mwenye ualbino kujeruhiwa

9 May 2024, 3:36 am

Sehemu ya majeraha aliyopata mtoto baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana.

Tukio la kujeruhiwa mtoto (10) mwenye Ualbino mkazi wa mtaa wa Mtakuja kata ya Katoro wilayani na mkoani Geita limekiibua Chama cha watu wenye Ualbino (TAS) wilaya ya Geita.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Katibu wa TAS wilaya ya Geita ameeleza hatua stahiki zilizochukuliwa na chama hicho kufuatia tukio hilo pamoja na mikakati ya kuwasaidia watu wenye Ualbino ili kujilinda na watu wenye nia ovu dhidi yao.

Sauti ya Katibu wa TAS

Viongozi wa waganga wa tiba asili kwa kanda ya ziwa wametoa tamko lao kuhusu maoni mseto yanayoendelea katika jamii ambapo vitendo hivyo huhusishwa na imani za kishirikina.

Sauti ya viongozi wa waganga

Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo alieleza kuwa majeraha ya mtoto na silaha iliyokutwa eneo la tukio ni wazi aliyefanya tukio hilo hakuwa na lengo la kuondoka na kiungo chochote.

Sauti ya Kamanda Geita