Storm FM

Geita All Stars bingwa Dimbani Cup 2023

13 August 2023, 12:11 pm

Fainali ya Dimbani Cup. Picha na Zubeda Handrish

Agosti 5, 2023 ligi ya Dimbani Cup ilianza rasmi ikishirikisha timu nane na kuanzia hatua ya mtoano na kukamilishwa na mshindi wakwanza na wapili.

Na Zubeda Handrish- Geita

Ligi ya Dimbani Cup 2023 inayofanyika chini ya kituo cha redio cha Storm FM kilichopo Mtaa wa Nyerere Road, kata ya Kalangalala, halmashauri ya mjini Geita, mkoani Geita, imekamilika rasmi leo Agosti 13, 2024 katika Dimba la shule ya sekondari Kalangalala baada ya matukio mbalimbali na kukamilishwa na fainali kati ya Geita All Stars dhidi ya Geita Veterani.

Fainali ya Dimbani Cup. Picha na Zubeda Handrish
Sauti ya mtangazaji wa Storm FM Zubeda Handrish akizungumzia kukamilika kwa Dimbani Cup

Geita All Stars wameibuka Mabingwa wa ligi hiyo kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya mechi kuisha kwa bao 1-1, Huku mshindi wa kwanza akiondoka na shilingi laki sita na jozi ya jezi, na mshindi wa pili shilingi laki nne na jozi ya jezi kamili na mgeni rasmi akitoa mipira miwili kwa mshindi wa kwanza na wa pili.