Storm FM

Kinababa pelekeni watoto kwenye chanjo

16 February 2024, 2:44 pm

Uzinduzi wa zoezi la utoaji wa chanjo ya Surua Rubella kituo cha afya katoro Mkoa wa Geita

Jamii imetakiwa kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo ili kuwakinga na maradhi mbalimbali.

Na Mrisho Shabani:

Kina baba Mkoani Geita wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miaka mitano kupatiwa chanjo ya surua na rubella kwakuwa suala hilo siyo la wanawake pekee.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela kwenye zoezi la uzinduzi wa kampeni ya utoaji wa chanjo ya surua na rubella katika mamlaka ya mji Mdogo wa Katoro wilayani Geita huku katibu tawala wa mkoa wa Geita Mohamed Gombati akizitaka halmashauri zote kuhakikisha zinaongeza kasi ya utoaji wa chanjo ili kufikia lengo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa kwenye uzinduzi wa zoezi la chanjo ya Surua na Rubella Mkoani humo.
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Katibu tawala wa Mkoa

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la utoaji wa chanjo hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt Omary Sukari amesema limeanza Februari 15 hadi 18 mwaka huu na wamelenga kuchanja watoto 517,798 kwenye vituo 622 mkoa mzima.

Sauti ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita

Baadhi ya wazazi waliojitokeza katika zoezi hilo Shinje Semando na Roda Hamisi wametoa wito kwa kina baba kutambua umuhimu wa kushirikiana na wenza wao katika malezi na makuzi ya mtoto.

Sauti ya Wazazi na walezi