Storm FM

Watumishi waliohama vituo vya kazi kwa uhamisho feki kufutwa kazi

13 September 2023, 8:23 pm

Watumishi wa umma wa wilaya ya Geita wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora. Picha na Mrisho Sadick

Uchunguzi umeanza kufanyika kwa watumishi wa umma waliohama vituo vyao vya kazi kwa njia za udanganyifu nakukimbilia mjini.

Na Mrisho Sadick – Geita

Serikali imesema itawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafuta kazi baadhi ya watumishi wa umma waliotumia nyaraka feki za uhamisho wa vituo vya kazi kinyume na taratibu,sheria na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe George Simbachawene wakati akisikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa umma na taasisi binafsi wa wilaya ya Geita katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. 

Sauti ya Waziri Simbachawene
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe George Simbachawene akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Geita. Picha na Mrisho Sadick

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ametembelea mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Inyala uliyotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi nakuridhishwa na utekelezai wa mradi huo huku akisema serikali imetoa kiasi cha Bilioni 70 Mkoani Geita kwa ajili ya wanufaika wa TASAF. 

Baadhi ya wanufaika wa TASAF Katika Kijiji Cha Inyala wilayani Geita Suzana Juma na Melesiana Masanja wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwaondoa katika umasikini kupitia TASAF.

Wakazi wa kijiji cha Inyala Geita wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya wanufaika wa TASAF

Waziri Simbachawene yupo Mkoani Geita kwa ziara ya siku tatu ya kusikiliza changamoto mbalimbali za watumishi wa umma , kuona Maendeleo ya wanufaika wa TASAF pamoja na miradi inayotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.