Storm FM

Polisi Geita: Mikopo ya pikipiki iende sambamba na mafunzo ya udereva

7 November 2023, 6:30 pm

Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Geita Mrakibu wa Polisi Aloyce akizungumza na Storm FM. Picha na Mrisho Sadick

Ajali za barabarani zaliibua Jeshi la Polisi juu ya mikopo holela ya pikipiki kwa vijana isiyozingatia usalama wao.

Na Mrisho Sadick – Geita

Jeshi la Polisi mkoani Geita limezitaka kampuni na watu binafsi wanaotoa mikopo ya pikipiki kwa vijana kuingia makubaliano na vyuo vya mafunzo ya udereva  ili vijana wanaoomba mikopo hiyo waweze kupatiwa mafunzo kabla ya kupewa vyombo hivyo ili kupunguza ajali za barabarani.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani mkoa wa Geita Mrakibu wa Polisi Joachim Aloyce wakati akizungumza na viongozi wa umoja wa waendesha Pikipiki Mkoa wa Geita ili kubaini changamoto zinazowakabili huku mwenyekiti wa umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Geita Carlos Ndagiwe akiomba mchakato huo uanze haraka ili kuwasaidia vijana.

Sauti ya RTO na Mwenyekiti wa Bodaboda Geita
Baadhi ya viongozi wa bodaboda mkoani Geita wakiwa kwenye kikao na Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha mapinduzi CCM Wilaya ya Geita Michael Msuya amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya sita nikuweka Mazingira rafiki kwa waendesha Pikipiki hapa nchini.

Sauti ya Katibu wa CCM