Storm FM

Wafutwa kazi kwa kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa kumwagiana dripu

3 December 2023, 9:28 pm

Mkurugenzi wa Hospitali ya Sakamu iliyopo Geita, Dokta Salvatory Kaaya Msimu

Wafanyakazi wawili wa Hospitali ya Sakamu wamezua taharuki kwa kusheherekea kwa furaha siku ya kuzaliwa ya mwenzao kwa kutumia majitiba maarufu ‘dripu’.

Na Said Sindo- Geita

Wafanyakazi watatu wa hospitali binafsi ya Sakamu iliyopo eneo la Magereza, mtaa wa Katoma, mjini Geita wamesimamishwa kazi huku uchunguzi ukianzishwa kuhusu video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Uongozi wa Hoapitali ya Samaku umekiri kuwa watumishi walio kwenye video hiyo ni wa Hospitali Binafsi ya Sakamu iliyopo Geita.

Sauti ya Mkurugenzi wa Hospitali ya Sakamu iliyopo Geita, Dokta Salvatory Kaaya Msimu

Tukio hilo lilitokea Desemba 1, 2023 na awali iliaminika kutokea katika Kituo cha Afya cha Nyankumbu, lakini baadaye imethibitika kuwa katika Hospitali ya Sakamu kufuatia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Salvatory Musimu.

Kwa upande wa Wizara ya afya imeupongeza Uongozi wa Hospitali hiyo kwa kuchukua hatua za haraka za uwajibishaji huku ikiendelea kuwakumbusha watumishi wa Afya kuzingatia maadili ya taaluma zao na kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.