Storm FM

Moto walipuka nakuteketeza vitu vyote vya ndani

2 April 2024, 5:24 pm

Ni sehemu ya uharibifu wa mlipuko wa moto katika nyumba ya Mathius Jeremiah. Picha na Kale Chongela

Katika hali isiyo ya kawaida moto ambao haukufahamika chanzo chake umelipuka na kuteketeza vitu vyote vya ndani katika nyumba ya bwana Mathius Jeremiah mkazi wa mtaa wa 14 Kambarage mjini Geita.

Na Kale Chongela – Geita

Vitu vya ndani katika nyumba ya Bw. Mathias Jeremiah mkazi wa mtaa wa 14 Kambarage kata ya Buhalahala mjini Geita vimeteketea kwa moto huku chanzo cha moto kikiwa bado haijafahamika.

Baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio  wamesema majira ya saa nne asubuhi tarehe 1 April ilisikika sauti ikiomba msaada katika Nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikiwaka moto jambo ambalo liliwalazimu kutafuta namba ya Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa hatua zaidi ya uokozi

Sauti ya Mashuhuda

Mama wa nyumba hiyo ambaye ametambulika kwa jina la Sarah Mathias amesema  wakati tukio linatokea yeye hakuwepo nyumba bali alikuwa soko la shilabela huku akishangazwa na tukio hilo la moto kuteketeza vitu vyake vya ndani

Sauti ya mhanga

Afisa habari na mawasilino kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Staff Sagernt Bahati Lugodisha amesema baada ya kupokea taarifa walifika eneo la tukio na kuanza kuzima moto huo ambapo ilichukua muda wa dakika 15 zoezi lilikuwa limekamilika la kuzima  moto ambapo amesema hadi sasa bado chanzo cha moto huo hakijafahamika 

Sauti ya afisa habari zimamoto