Storm FM

Wananchi zaidi ya laki 6 wanufaika na mradi wa maji Geita

28 August 2023, 9:07 am

Changamoto ya kupatikana kwa maji safi na salama vijijini, imechangia kwa kiasi kikubwa mradi wa maji wa miji 28 kuanzishwa.
Na Adelina Ukugani- Geita
Jumla ya wakazi laki sita na thelathini na nane mia tatu na ishirini na  mbili (638,322 ) wanatarajia kunufaika na mradi wa maji wa miji 28 , ambapo jumla ya kata 19 na vijiji 19 vilivyopo Wilayani Geita vinatarajia kupata manufaa ya uwepo wa mradi huo wa maji ambao unajengwa kwenye Kata ya Senga Wilayani humo.

Hii ni baada ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kukagua miradi  na kufika kwenye eneo ambalo ndipo linatarajia kuanza ujenzi wa mradi huo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mhadisi Isaac Mgeni kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira  Mjini Geita (GEUWASA)ameelezea hatua za awali ambazo wanaendelea nazo.

Sauti ya Mhadisi Isaac Mgeni kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira  Mjini Geita (GEUWASA)

Diwani wa kata ya Senga Thomas Tumbo, amedai changamoto iliyopo ni wananchi kuthaminiwa na kulipwa fidia kwa wale ambao mashamba yao yatapitiwa na mradi.

Sauti ya Diwani wa kata ya Senga Thomas Tumbo

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Geita, Mjumbe wa  Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Humo, Taitus Kabuo amesisitiza ni vyema kwa fidia ikafanywa haraka ili iweze kulipwa  kwa wananchi ambao mradi utawapitia.

Sauti ya Mjumbe wa  Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Geita,Taitus Kabuo.

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita, imefanya ziara katika wilaya mbalimbali mkoani hapa na kufanya ukaguzi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.