Storm FM

Chanjo ya Polio kutolewa kwa awamu ya pili mkoani Geita

4 May 2026, 4:59 pm

Mratibu wa elimu ya Afya kwa UMMA Geita Bi. Paskazia Madulu akizungumza na Storm FM. Picha na Ester Mabula

“Mafanikio ya awamu ya kwanza yalifikia zaidi ya asilimia 100 na tunatarajia hata kwa awamu hii ya pili zoezi letu litakwenda kikamilifu ili watoto waweze kupata chanjo” – Mratibu wa elimu ya Afya kwa UMMA Geita Bi. Paskazia Madulu

Na: Ester Mabula

Serikali kupitia wizara ya Afya inatarajia kuanza kutoa chanjo ya Polio kwa awamu ta pili kwa watoto chini ya umri wa miaka 10 mkoani Geita tangu kukamilika kwa awamu ya kwanza ya utoaji wa chanjo hiyo Marchi 27, mwaka huu.

Maandalizi ya mpango huo yameambatana na utoaji wa elimu kwa watu maarufu kwenye Jamii iliyotolewa leo Mei 04, 2026 ambao wameelishwa juu ya umuhimu wa chanjo hiyo, akizungumza muelimishaji  Penford Joel kutoka wizara ya Afya idara ya kinga sehemu ya Afya kwa UMMA amesema awamu hii ya pili itatolewa kwa watoto wote hata ambao waliopata chanjo awamu iliyopita.

Sauti ya Penford Joel kutoka wizara ya Afya
Penford Joel kutoka wizara ya Afya idara ya kinga sehemu ya Afya kwa UMMA. Picha na Ester Mabula

Mratibu wa elimu ya Afya kwa UMMA mkoa wa Geita Bi. Paskazia Madulu amesema awamu ya kwanza zoezi hilo lilifanyika kikamilifu na hivyo wana matarajio makubwa kwa awamu ya pili ambayo itaanza Mei 7 hadi 10 mwaka huu huku Mratibu wa Redcross mkoa wa Geita Peter Enock akiwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo

Sauti ya waratibu, Paskazia Madulu na Peter Enock

Baadhi ya washiriki waliopewa elimu hiyo wameeleza kuwa watasaidia kuielimisha Jamii juu ya umuhimu wa chanjo huku wakiipongeza serikali kwa kuendelea kutoa elimu ya kupambana na maradhi mbalimbali.

Sauti ya washiriki waliopata elimu
Mratibu wa Redcross mkoa wa Geita Peter Enock akizungumza na Storm FM. Picha na Ester Mabula