Storm FM

BUCKREEF kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti

26 September 2023, 7:27 pm

Afisa usalama, afya na mazingira kutoka Mgodi wa Buckreef Bw. Chales Kafuku. Picha na Kale Chongela

Mgodi wa BUCKREEF umeendelea kupanua wigo katika kuzalisha miche ya miti ili kuhakikisha mazingira yanaendelea kutunzwa katika kupanda miti maeneo yanayozunguka mgodi.

Na Kale Chongela- Geita

Katika kuendelea kutatua changamoto ya uharibifu wa mazingiara ikiwemo ukataji miti kiholela, Mgodi Wa Buckreef umeanda kitalu chenye miche elfu kumi na Tano ikiwa lengo ni kutunzia mazingiara kwa kupanda miti.

Wafanyakazi wa BUCKREEF katika maonesho ya 6 ya kimataifa ya teknolojia ya madini. Picha na Kale Chongela

Hayo yamebainishwa na afisa usalama, afya na mazingira kutoka Mgodi wa Buckreef Bw. Chales Kafuku ambapo amesema lengo ni kuendelea kutunzia mazingira.

Sauti ya afisa usalama, afya na mazingira kutoka Mgodi wa Buckreef Bw. Chales Kafuku

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira Mhe. Selemani Jafo Ametumia fursa hiyo kwa kuwataka kuendelea kuweka vitalu kwenye maeneo ya shule sambamba na maeneo ambayo yanazunguka Mgodi huo.