Storm FM

Aonekana hai baada ya kufariki miaka 3 iliyopita Geita

4 January 2024, 11:12 am

Mwanamke Mugumba Misalaba aliyepatikana akiwa hai Fitina baada ya kufariki miaka 3 iliyopita. Picha na Amon Bebe

Matukio ya baadhi ya watu kufariki dunia na kuonekana tena yameendelea kutokea katika maeneo tofauti, jambo ambalo linazua mizozo na kuhusishwa na imani za kishirikina.

Na Amon Bebe- Geita

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mugumba Misalaba ambaye alifariki Dunia miaka mitatu iliyopita na kuzikwa katika Kijiji cha Nyakato, Kata ya Nyanguku, Wilayani Geita amezua gumzo baada ya kuonekana kijijini hapo akiwa hai.

Sauti ya Mugumba Misalaba aliyepatikana akiwa hai Fitina

Kwa mujibu wa kaka yake Fitina Misalaba amesema dada yake alifariki tarehe 15 mwezi wa tisa mwaka 2020 kwa ajali ya gari na wakamzika tarehe 17 ya mwezi huo, Lakini cha kushangaza ni kwamba tarehe 01/01/2024 walipata taarifa kutoka kwa baadhi ya wanakijiji kuwa wamemuona na walipofika alipo wakagundua kweli ni yeye.

Sauti ya kaka wa Mugumba Misalaba aliyepatikana akiwa hai Fitina Misalaba

Diwani wa kata hiyo ya Nyanguku Elias Mlole nae amezungumza alivyolifahamu tukio hilo na familia hiyo.

Sauti ya Diwani wa kata hiyo ya Nyanguku Elias Mlole

Mkuu wa wilaya ya Geita Mheshimiwa Cornel Magembe amewataka wananchi wa Kijiji hicho kuwa na utulivu na kama kuna watu wanafanya mambo ya kishirikiana ya kuwatesa watu kiasi hicho waache tabia hiyo mara moja kwani haipendezi na haikubariki kabisa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita Mheshimiwa Cornel Magembe