Storm FM

Vibubu vyaboreshwa kuendana na soko

21 August 2023, 9:06 am

Vibubu vya asili. Picha na Zubeda Handrish

Inadaiwa kibubu hakiwezi kutoa usalama wa moja kwa moja kama benki, huku kikidaiwa kupoteza fedha zilizohifadhiwa ndani yake , hili limewainua wauza vibubu na kutolea ufafanuzi.

Na Zubeda Handrish- Geita

Mfanyabiashara wa Vibubu katika soko la Nyankumbu la jioni amezungumzia namna vibubu vinavyonunuliwa kwa wingi katika eneo lake na zaidi wanawake wakivunja rekodi.

Sauti ya mfanyabiashara wa vibubu vya asili

Kutokana na kukua kwa soko la Vibubu kwa kununuliwa na watu wa kaliba tofauti, baadhi ya wabunifu wameviongezea thamani zaidi kwa kuvitengeneza kwa muonekano wa kuvutia.

Sauti ya mfanyabiashara wa vibubu vya kisasa
Vibubu vya kisasa. Picha na Zubeda Handrish

Nao baadhi ya wananchi mjini Geita, wamesemaje wanatumia vibubu ili kuwekeza pesa kidogo kidogo kwaajili ya kutimiza malengo yao.

Sauti ya wananchi wa Geita mjini wakizungumzia matumizi ya kibubu

Tukamilisha hapa na meneja wa moja ya benki mjini Geita akielezea umuhimu wa kutunza pesa katika taasisi za kifedha hususani benki.

Meneja Biashara NBC Geita, Ally Iddi

Ili kuepuka madhara haya, ni bora kuweka fedha zako katika taasisi za kifedha zilizosajiliwa kisheria, kama vile benki. Benki zinatoa usalama zaidi na fursa za uwekezaji na faida zingine.
Kama unataka kuwekeza au kufanya uwekezaji wa muda mrefu, unaweza pia kuzingatia chaguzi za uwekezaji zilizoainishwa vizuri na wataalamu wa kifedha.