Storm FM

Wanufaika wa Tasaf Geita wapewa ushauri

15 April 2021, 6:15 pm

Na Elizabeth Obadia

Wakazi wa mtaa wa nyamalembo wanaonufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini tanzania tasaf wameshauriwa kuzitumia vizuri pesa wanazozipata kwa kufanya uwekezaji ili kujiongezea kipato zaidi.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa nyamalembo Bw. Bahati Gulaka wakati wa zoezi la ugawaji wa pesa za tasaf na kuelezea namna anavyohakikisha wanufaika wanapata pesa zao kama inavyotakiwa

Mwenyekiti wa Mtaa

Nao baadhi ya wanuafaika wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini wameelezea namna ambavyo wameweza kunufaika na pesa wanazozipata.