Storm FM

Waendesha vyombo vya moto walia ongezeko bei ya mafuta

2 August 2023, 1:50 pm

Waendesha vyombo vya moto mjini Geita. Picha na Zubeda Handrish

Siku chache zilizopita ilitokea changamoto ya uhaba wa mafuta ya petroli na dizeli mkoani Geita na Tanzania, licha ya Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba kuthibitishiwa kuwepo kwa mafuta ya kutosha kwenye maghala ya kuhifadhia mafuta nchini.

Na Zubeda Handrish- Geita

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zilizoanza kutumika kuanzia leo Jumatano August 2, 2023 saa 6:01 usiku.

Afisa Tawala Msaidizi Huduma kwa Wateja EWURA CCC mkoa wa Geita, Wadi Omary amethibitisha kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa, huku akiainiasha bei kwa mkoa wa Geita.

Sauti ya Afisa Tawala Msaidizi Huduma kwa Wateja EWURA CCC

Afisa Tawala Wadi amesema kuna sababu nyingi zilizopelekea mafuta kupanda, huku akiwasihi watumia vyombo vya moto kutoa taarifa endapo watakutana na bei kubwa zaidi ya elekezi.

Afisa Tawala Msaidizi Huduma kwa Wateja EWURA CCC. Picha na Zubeda Handrish
Sauti ya Afisa Tawala Msaidizi Huduma kwa Wateja EWURA CCC

Nao baadhi ya waendesha vyombo vya moto mkoani Geita wamezungumzia juu walivyoguswa na bei hizo huku wakilia na hali ya kiuchumi.

Sauti ya mwendesha chombo cha moto mjini Geita
Sauti ya muendesha chombo cha moto mjini Geita

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei kunatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola ya Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.