Storm FM

Storm FM yaendelea kujengewa uwezo na TADIO

14 July 2023, 4:05 pm

Waandishi wa Habari wa Storm FM wakiwa katika mafunzo ya Redio Portal. Picha na Mrisho Sadick

Mtandao wa Redio Jamii wa TADIO umeendelea kuziimarisha redio hizo kwendana na wakati hususani katika kurusha matangazo kwa njia ya mtandao.

Na Mrisho Sadick:

Mtandao wa TADIO umeendelea kuijengea uwezo Storm FM wa namna ya kutumia mtandao wa Redio Portal kuyafikia makundi yote katika Jamii kutokana na kukua kwa teknolojia na watu wengi kutumia mtandao.

Mhariri Mkuu wa Redio Portal Hilali Ruhundwa akiwa katika kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita akitoa mafunzo kwa vitendo ya namna ya kutumia jukwaa hilo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa kituo hicho, amesema wanalazimika kutoa mafunzo hayo kutokana na kukua kwa teknolojia inayochangia idadi kubwa ya watu kutumia mtandao.

Amesema katika jukwaa hilo la Redio Portal unaweza kupata habari kupitia vyanzo vingi ikiwemo kwa sauti , maandishi na picha.

Mhariri wa Redio Portal Hilali Ruhundwa akitoa mafunzo Storm FM. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mhariri wa Redio Portal Hilali Ruhundwa

katika hatua nyingine Hilali amewasihi wakuu wa vituo vya Redio wanachama wa TADIO wakiwemo wahariri kuendelea kueneza mafunzo hayo kwa waandishi wa habari wengine katika vituo vyao ambao hawajapata nafasi hiyo ili kuhakikisha jukwaa hili la Redio Portal linakuwa imara zaidi.

Sauti ya Mhariri wa Redio Portal Hilali Ruhundwa