Storm FM

Watu watano wamenusurika kifo baada ya lori kugonga nyumba

4 September 2023, 11:54 am

Mwonekano wa Lori lilivyo paramia nyumba. Picha na Amon Bebe

Taharuki yaibuka baada ya Lori kugonga nyumba nyakati za usiku katika Mtaa wa Kivukoni Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita.

Na Mrisho Sadick:

Watu watano wamenusurika kifo baada ya Lori la mchanga lenye namba za usajili T 665 DWF kugonga Nyumba katika Mtaa wa kivukoni Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo baada ya gari hilo kuparamia nyumba hiyo huku chanzo chake kikiwa bado hakijafahamika , baadhi ya manusura na mashuhuda Ester Mwita na Ridia Alex wamezungumzia  tukio hilo.

Sauti ya manusura na shuhuda

Mmiliki wa Nyumba hiyo Grace Masolwa amesema uharibufu uliyofanyika unagharimu zaidi ya milioni 20 huku balozi wa Mtaa huo Samson Jeremia akieleza hatua zilizochukuliwa.

Sauti ya mmiliki wa Nyumba na Balozi